المدة الزمنية 1:1:51

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA: IBADA MORNING GLORY DEC 04, 2020

8 112 مشاهدة
0
150
تم نشره في 2020/12/04

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA: IBADA YA MORNING GLORY DEC 04, 2020 UJUMBE WA LEO: "VITA YA NDOTO" "VITA YA NDOTO" (WAUA NDOTO) DREAM KILLERS Mwanzo 37 : 5 -8 , 20 Danieli 6 : 4 - 5 Mwanzo 37 : 5 -8 , 20 5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; 6 akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. 7 Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. 8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. 20 Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake. Danieli 6 : 4 - 5 4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. 5 Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake. Mhubiri: Mwl. Eng. Goodluck Mushi Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 68