المدة الزمنية 5:38

Dalili za Mimba ya Mtoto wa Kike Tumboni mwa Mjamzito | Ni zipi Dalili za Mimba ya Mtoto wa Kike.

بواسطة Dr. Mwanyika
90 286 مشاهدة
0
804
تم نشره في 2021/12/05

Kumekuwa na imani nyingi kuhusu Dalili za Mimba ya Mtoto wa Kike katika Mimba Changa na Akina mama wengi wajawazito wanakuwa na shauku kubwa kujua jinsia za watoto wao waliopo tumboni mapema kabla ya kujifungua. 📌Kwa hizo imani kama una watoto mapacha dalili za Mama Mjamzito zitakuwaje 😆😆😆😆??? Mojawapo ya imani hizo ni kama; 1. Mimba ya Kike huwepo endapo Mama mjamzito akiwa na dalili za kutapika au kichefu chefu ahsubuhi Zaidi na kinyume chake huwa ni Mtoto wa Kiume. ✅Comment yangu; Hakuna ukweli wa kisayansi kuhusu hili kwani dalili za kutapika huathiriwa na mabadiliko ya homoni na pia huweza kusababishwa na shida nyingine kama Gestational Trophoblastic Diseases ambapo Mama ana weza tapika sana na akahisi mtoto wa kike kumbe siyo mtoto kabisa! 2. Tumbo la Mama Mjamzito mwenye Mtoto wa Kike Tumbo huwa juu zaidi na hii kinyume na Mtoto wa Kiume ambapo Tumbo huwa chini zaidi. ✅Comment yangu; Hakuna ukweli wa Kisayansi kwani mkao wa tumbo huathiriwa na maumbile ya mfuko wa uzazi wa Mama husika na hutofautiana kati ya Mama mmoja na mwingine. 3. Mama Mjamzito mwenye Mtoto wa Kike tumboni mabadiliko ya mood huwa ni zaidi kuliko yule mwenye Mtoto wa Kiume ambapo huwa ana mabadiliko ya Mood kidogo tuu. ✅Comment yangu; Hakuna ukweli wa kisayansi kwani mabadiliko ya Mood huathiriwa na mabadiliko ya homoni na siyo Jinsia ya mtoto. 4.Mama mwenye Mtoto wa Kike Tumboni hupendelea kula vyakula vitamu Kama chocolate, Pipi wakati mwenye Mtoto wa Kiume hupendelea vyakula vichungu kama ukwaju,Ndimu mbichi na Nyanya chungu tofauti. ✅Comment yangu: Hakuna ukweli kwani mabadiliko ya radha huathiriwa na mabadiliko ya homoni na siyo jinsia ya Mtoto wa Kiume au Kike. 5. Mama mjamzito mwenye mtoto wa Kike huwa na chunusi na madoa madoa usoni wakati Mtoto wa Kiume Mama huwa Mzuri katika ngozi yake. ✅Comment yangu: Hakuna ukweli wa kisayansi kwani mabadiliko ya ngozi huathiriwa na mabadiliko ya homoni na siyo jinsia za watoto. 6.Mama mwenye mtoto wa Kike Tumboni mapigo ya Moyo ya mtoto huwa zaidi ya 140Bpm ukilinganisha na yule wa Kiume ambapo huwa chini ya 140Bpm. ✅Comment yangu: Hakuna ukweli kwani mapigo ya Moyo ya mtoto huathiriwa na vitu vingi na siyo jinsia ya mtoto. Kwa hizo imani je kama una watoto mapacha je itakuwaje😆😆😆😆😆😆😆? ✅UKWELI WA KISAYANSI✅ ❤️Unataka kujua jinsia ya mwanao hakikisha ukifikisha wiki 20 kwenda juu(miezi 5) yaa ujauzito, uende hospitali na ufanyiwe ultrasound hiyo itakuonesha jinsia ya Mtoto wako kwa uhakika Lakini hutegemea zaidi mtalamu wa Ultrasound na Mkao wa Mtoto Tumboni mwa Mjamzito. Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp ©Dr.Mwanyika #drmwanyika #mamaafya #MtotowaKike

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 284